Msanii wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi.
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutumika kwa utapeli kupitia namba yake ya simu.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Snura alisema aliacha kutumia namba ya awali kwa muda wa miezi miwili baada ya kupotea ambapo hivi karibuni ndipo alipoanza kupata malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali kwamba anawaomba fedha kwa madai kwamba mama yake anaumwa.
“Kuna mtu sijui alifanyaje mpaka akawa anaitumia hiyo namba kibaya zaidi anatapeli watu hela na kujifanya ni mimi, imeniuma sana jamani mimi sijamuomba mtu yeyote hela na hiyo namba siitumii tena kuweni makini na huyo tapeli,” alisema Snura.