Aibu ya kufunga mwaka! Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, amesimamia fumanizi la dada’ke ambaye ni denti wa sekondari moja jijini Dar (majina yanahifadhiwa kwa sababu maalum) ambapo alimfumania chumbani na njemba mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa Mbagala-Charambe, Dar.
OFM ikiwa kazini, ilipokea malalamiko kutoka kwa Nicholaus aliyedai kwamba amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba kila ikifika saa 2: 00 usiku kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na kuingia chumbani kulala na mdogo wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri.
Nicholaus alisema kuwa mara nyingi vitendo hivyo hufanyika wikiendi ambapo katika kuhangaika kumnasa anayemharibu mdogo wake aliwataarifu OFM ambao waliingia mzigoni na kuweka mtego uliomnasa sharobaro huyo.
OFM hawakuwa wenyewe kwani walimtaarifu Mjumbe wa Mtaa wa Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo akatoa ushirikiano uliofanikisha kumnasa Abuu.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Waraka wa kujikomiti wa Sharo alioundika mbele ya mjumbe, Hawa Ally.
OFM walisubiri kwa muda wa robo saa kisha wakaingia ndani ya nyumba hiyo kwa msaada wa wapangaji na kumnasua binti huyo ili aendelee na masomo.Sharobaro huyo alikiri kuingia mara kadhaa ndani humo na kubanjuka na denti huyo.
Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa, pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.