MKAZI
wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani
Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu ya sura
yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.
Mtoto
huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu
Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa.
Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Kwa
mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya
mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao
haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida
licha ya njia ya uzazi kufunguka.
Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto.
Alisema
wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima miezi ya
mwisho mama huyo, mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani pamoja na mapigo ya
moyo lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa
likiwashangaza waganga na wauguzi kituoni hapo.
Dk
Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji waliweza
kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambaye alikuwa na sura isiyoeleweka na
kichwa kilikuwa na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni sura inayofanana na
chura huku viungo vingine vyote vya mwili vikiwa kamili.
Alisema
zipo sababu kadha zinazoweza kusababisha tatizo kama hili ambapo
alisema kuwa ni baadhi ya akinamama kukosa baadhi ya madini mwilini na
uumbaji kutokamilika kutokana na sababu za kibaiolojia.
Alieleza kuwa hali ya mama huyo inaendelea vizuri na kwamba mtoto huyo alikuwa ni mtoto wake wa tano