Hatma
ya rapper Chidi Benz kuhusiana na kama ataachia huru au kufungwa jela
kutokana na mashtaka matatu yanayomkabili kufuatia kukamatwa na madawa
ya kulevya, haikuweza kujulikana Alhamis hii baada ya kupanda tena
kizimbani kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Chidi
amepangwa kurejea tena mahakamani hapo January 15, 2015. Juzi rapper
huyo alikuwa na imani kuwa Alhamis hii angeweza kujua hatma yake na pia
kuwaomba watu wamkumbuke kwenye sala.
“Kesho (jana) ni judgement yangu na ni mwisho wa kesi yangu pale kwa hakimu mkazi Kisutu,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Najua
nimekosea lakini sio sana kuliko makosa yote,muhimu ni kusamehe na
kuondoa hasira na mimi,msipoteze Imani na mimi,nimekua msanii mzuri na
bora kwa kipindi choote..nikiwa kazini inafahamika nachokifanya,sijawai
kosea kuifanya kazi yangu hayo mengine ni mengine tayari..mnaweza
kutokea kwa Sapot na naomba Mniombee.nisirudi kuule.Tafadhar.”