Mdogo
wake na Zari Hassan aka The Bosslady, aitwaye Karim ametumia Facebook
kumkosoa dada yake kwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz ambaye
anamzidi miaka 9.
Kwenye post hiyo, Karim aliandika: You are ashaming us, how can you date a boy my age. You moved from one man to another in less than 3 days.”
Akitumia akaunti yake binafsi ya Facebook yenye jina ‘Zarinah Tlale’,
kujibu post hiyo ya mdogo wake huyo ambaye hapendezwi na kitendo cha
dada yake kuwa na uhusiano na mtu mwenye umri kama wake, Zari alisema si
Karim aliyeiandika.
“Diamond
is just a friend of mine. It’s never been written that female and male
can’t be friends, it’s just the backward people that use that kind of
perspective to blow things out of proportion,” aliandika.
Katika
hatua nyingine baada ya kumsindikiza Diamond kwenye tuzo za Channel O,
Jumamosi iliyopita, Zari alimpa kampani pia kwenye utengenezaji wa video
ya wimbo alioshirikishwa na kundi la Nigeria, Bracket.
Chanzo: Uganda Online