Jacqueline Wopler (kushoto) akibeba mfuko wa sukari.
Vyakula vilivyotolewa na Jacqueline Wolper katika kituo cha kulelea wazee wasiojiweza kituo cha Msimbazi Centre jijini Dar.
Sister Wilbroda Mangwangi (katikati) na Wolper wakisalimiana.
Wolper akisalimiana na Bibi Rachel Christopher.
Mpishi wa wazee Salma Hamidu.
Wolper akimsalimia mzee ambaye hajiwezi.
Wolper akisaini kitabu cha wageni.
Woper Family.
KATIKA kuadhimisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake , msanii wa
filamu nchini hapa Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ ametoa msaada kwa
wazee wasiojiweza kituo cha Msimbazi Centre jijini Dar, ambacho kiko
chini ya kanisa Katoliki.Kabla ya kutoa msaada huo Wolper alisoma dua nyumbani kwake na baadaye kwenda katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula kama Mchele kg 100, Unga wa sembe kg 50, sukari kg 100 na mafuta ya kula madumu mawili.
(Picha na Shani Ramadhani/GPL)