Diamond anakwenda mbele zaidi kwa kukumbuka maneno makali na yenye kuchoma moyoni ambayo aliambiwa na demu huyo ambapo kila akiyakumbuka hata leo, bado haamini kilichotokea!
“Nakumbuka siku hiyo yule demu aliniambia, ’sikiza Diamond, mi’ kwa sasa siwezi kuwa na mwanaume ambaye hana masilahi kwangu.’
Neno ‘mwanaume ambaye hana masilahi kwangu lilimuumiza nyota huyo kwani aligundua kumbe ulimwenguni ili upate vitu vizuri ni lazima uwe na fedha kwa vile yeye hakuwa na ‘mpunga’, demu alimtoka hivihivi anajiona.
Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Platnamuz au ‘Sukari ya Warembo’ anasema mwaka 2009, alikutana na Peter Msafiri ‘Papaa Misifa’ ambaye alisema atamsaidia kumkuza kisanii mpaka atoke na kuwa tishio Bongo.
Diamond anasema akiwa na Papa Misifa alifanikiwa kurekodi Wimbo wa Nenda Kamwambie. Anasema:
“Huu wimbo nilimtungia Sarah, mpenzi wangu aliyenimwaga kwa sababu sikuwa na masilahi kwake (hivi karibuni amemwagwa na Wema Sepetu).“Nilimweleza kwenye wimbo ni kwa kiasi gani niliumia kwa kuniacha kwake wakati nilikuwa bado nampenda.”
“Huu wimbo nilimtungia Sarah, mpenzi wangu aliyenimwaga kwa sababu sikuwa na masilahi kwake (hivi karibuni amemwagwa na Wema Sepetu).“Nilimweleza kwenye wimbo ni kwa kiasi gani niliumia kwa kuniacha kwake wakati nilikuwa bado nampenda.”
Diamond anakiri kwamba, alianza kung’ara katika sanaa na wimbo huo na maisha yakabadilika kiasi cha kufika hatua ya kununua gari la kwanza kabisa aina ya Toyota Celica.
Februari 14, 2010, Diamond aliachia albamu yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo kumi. Nyimbo hizo ni Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Nalia na Mengi, Binadamu, Nakupa, Usisahau, Uko Tayari, Wakunesanesa, Toka Mwanzo na Jisachi.Anasema Aprili mwaka huohuo alikuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kushinda tuzo 3 za Tanzania Kili Music Awards.
Anazitaja tuzo hizo kuwa ni ya Msanii Bora Chipukizi, Wimbo Bora wa Mwaka (Kamwabie) na Wimbo Bora wa R&B (Kamwambie). Kama vile haitoshi, heshima ikapanda kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Malaria Tanzania.
Diamond anasema Wimbo wa Mbagala ulipendwa sana kwani mwaka huohuo ukiwa unavuma sana, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete ‘JK’ alimteua kuwa mburudishaji kwenye ziara za kampeni ya Uchaguzi Mkuu Rais, mwaka 2010 ambapo JK aliibuka kidedea.