Lionel Messi ahuzunishwa na mauaji ya watoto Gaza

Lionel Messi nyota wa timu ya soka ya Barcelona ya Uhispania na nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Argentina amesema kuwa, amesikitishwa mno na mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watoto katika Ukanda wa Gaza na kutoa wito wa kusitishwa vita na mauaji dhidi ya watoto wasio na hatia.
Messi ambaye ni “Balozi wa Nia Njema wa Umoja wa Mataifa” amelaani vikali mashambulio ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza. Mchezaji huyo mahiri wa Barcelona ameandika katika ukurasa wake wa facebook: “Hushikwa na huzuni na simanzi kila siku ninapoona picha za watoto wadogo wa Kipalestina wakiwa wameuawa.” Aidha ameandika katika ukurasa wake huo kwamba: Nikiwa baba na Balozi wa Nia Njema wa Umoja wa Mataifa, nimesikitishwa mno na mauaji dhidi ya watoto huko Gaza. Vita hivi vimepelekea watoto wengi kuuawa na maelfu ya watoto wengine kujeruhiwa.” Aidha Lionel Messi amesisitiza kwamba, vita na utumiaji mabavu huo unapaswa kusitishwa. Ikumbukwe kuwa hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba, mchezaji huyo wa Barcelona ameupatia msaada wa fedha utawala wa Kizayuni wa Israel, madai ambayo yamekanushwa mchezaji huyo na kusisitiza kwamba, ataliburuza mahakani gazeti la Ufaransa lilichapisha habari hiyo.