HATA MATAIFA MAKUBWA NAYO YANAFELI?? CHEKI HIYOOOO Marekani yashindwa kukomboa raia wake Syria

 Marekani yashindwa kukomboa raia wake Syria

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo hivi karibuni lilifanya operesheni ya anga na nchi kavu ili kuwakomboa Wamarekani waliotekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Daesh nchini Syria lakini  halikufanikiwa. Msemaji wa Pentagon Admiral John Kirby ameeleza kuwa, operesheni hiyo haikufanikiwa kwani mateka hawakuwepo katika eneo walilolilenga. Imeelezwa kuwa, Rais Barack Obama ndiye aliyeamuru operesheni hiyo ya siri iliyofeli nchini Syria ili kuwakomboa Wamarekani wanaoshikiliwa na kundi la Daesh akiwemo mwandishi habari James Foley aliyechinjwa na kundi hilo.

Matamshi hayo yametolewa na maafisa wa Marekani siku moja baada ya kundi la ISIL kutoa video inayoonesha mwandishi habari James Foley akikatwa kichwa. Hata hivyo Rais Barack Obama amesema kuwa, Marekani itaendelea kufanya kila iwezalo kuwalinda raia wake akidai kwamba  kukatwa kichwa mwanahabari huyo kumethibitisha kuwa kundi la Daesh halina dini.
Ikumbukwe kuwa kundi hilo la kigaidi na mengine yanayopigana nchini Syria kwa karibu miaka mitatu sasa dhidi ya serikali ya nchi hiyo yamekuwa yakisaidiwa kwa hali na mali na nchi za Magharibi hususan Marekani na waitifaki wake wa Mashariki ya Kati kama Saudi Arabia an Qatar.