KUMENUKA ST.JOSEPH ARUSHA. MKONG'OTO WA TEMBEA!!!!!!!!

POLISI wametumia nguvu kuwatawanya wanafunzi Chuo Kikuu cha St. Joseph mjini hapa, waliofunga barabara ya kutokea Arusha kwenda Singinda katika eneo la Kisongo, wakilalamikia mitaala.

Katika tukio hilo wanafunzi 23 wanashikiliwa na wanaendelea kuhojiwa.

Tukio hilo lilitokea jana majira ya kuanzia saa 2:30 hadi saa 5:55 mchana na kusababisha magari yanayotumia barabara hiyo kushindwa kupita.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Liberatus Sabas, alithibitisha kukamatwa kwa wanafunzi hao na kusema wanaendelea kuwahoji.

Wanafunzi hao wa shahada ya kwanza na Diploma wanalalamikia kufundishwa mitaala ya nje hasa kutoka India na wanahofu kwamba wanaweza kukosa ajira baada ya kumaliza.

Mgomo wa wanafunzi hao umedumu kwa wiki moja sasa.