Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamng’ang’ania mfanyabiashara maarufu wa Wilaya ya Mvomero, Johnson Damian Mkude (39) akituhumiwa kumkata kichwa mdogo wake wa kuzaliwa, Mathias kisha kuondoka nacho kwenda kwa mganga kwa kile kilichodaiwa ni kufanyiwa dawa ili awe bilionea.
Tukio hilo ambalo kwa sasa ndiyo gumzo mkoani hapa lilijiri usiku wa Agosti 3, mwaka huu katika mashamba ya Kata ya Mlali ambapo ndugu wa marehemu waliokuwa wakimsaka ndugu yao walifanikiwa kuona kiwiliwili Agosti 6, mwaka huu.
BABA WA MAREHEMU
Akizungumzia tukio hilo kwa uchungu, baba wa marehemu mzee Mkude alisema:
”Mwezi mmoja kabla ya tukio, Johnson alinichonganisha na Mathias, nakiri hadi marehemu anakufa nilikuwa sina uhusiano naye mzuri kutokana na maneno aliyoniambia kaka yake.

“Lakini nilipomuuliza kuhusu hayo maneno, Mathias alikanusha, nikaamua kuyafanyia uchunguzi. Wakati naendelea na uchunguzi Agosti 3, mwaka huu, majira ya jioni, giza halijaingia niliwaona wanangu (Jonson na Mathias) wamepakizana kwenye bodaboda.
“Siku hiyohiyo, saa 5 usiku, mke wa Mathias, Revina Evarist akaja kwangu na kunijulisha kwamba mumewe hajarudi nyumbani na si kawaida yake kufika muda huo. Tulipompigia simu hakuwa hewani. Kwa vile nilimuona akiwa na kaka yake, nikampigia yeye lakini simu yake ilizimwa.
“Ilipofika saa 7 usiku tukaamua kwenda kwa kaka yake, tukamkuta. Nilipomuuliza mdogo wako yuko wapi akasema hajui. Akajiunga na sisi, tukaendelea kumtafuta mdogo wake kwa zaidi ya siku 2 bila mafanikio,” alisema mzee huyo.
MAITI YAONEKANA VIP?
Mzee huyo akasema Agosti 6, mwaka huu alipata taarifa kwamba kuna maiti imeonekana kwenye mashamba ya Mlali.
“Nilishtuka sana kusikia hivyo, nikamtuma mkwe wangu, mume wa mtoto wangu mkubwa na mtoto wa dada yangu, Gasper Msimbe. Walisafari hadi Kata ya Mlali kushuhudia maiti hiyo.
“Walipofika waliikuta maiti haina kichwa lakini walimtambua kuwa ni Mathias kwa nguo na viatu. Walinijulisha haraka ambapo nilikwenda eneo la tukio. Nilipofika niliumia sana kushuhudia mwanangu asiyekuwa na hatia kauawa kikatili huku mwili wake uliokuwa hauna kichwa ukitoa harufu kali kwa kuharibika.”
BABA AOMBA KICHWA CHA MWANAYE
“Pale kituoni, polisi walinitaka nimsalimie lakini nikakataa mpaka arudishe kichwa cha mdogo wake. Tena naliomba jeshi la polisi kumbana Johnson ili kama kweli amechukua kichwa cha mdogo wake akirudishe nikizike hapa nyumbani Kijiji cha Nyandila,” alisema mzee huyo