DAKTARI ADHURIKA NA EBOLA SEIRRA LEONA
DAKTARI aliye kuwa mstari wambele katika kupambana na ebola sasa yupo ICU kwa matibabu zaidi. Sheik Umar Khan alibainika kuwa na Virusi vya Ebola na sasa amelazwa katika hospitali moja mjini Kailahun ambapo ugonjwa huo umekua ukijitokeza kwa wingi.
Zaidi ya Watu 630 wamepoteza maisha katika nchi tatu za Afrika magharibi tangu mlipuko wa ugonjwa huo kuanza nchini Guinea mwezi Februari, takwimu za Umoja wa Mataifa zimeonesha.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchi hiyo zimesema Waziri wa Afya alikua akibubujikwa na machozi aliposikia taarifa za dokta Khan
Waziri wa Afya wa Sierra Leone Miatta Kargbo amemuita daktari huyo kuwa “shujaa wa taifa” na kusema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anapona.