Wabunge `walivyolilia` Sh. bilioni 100 wizara ya afya!!!!!!!

Wiki iliyopita wakati Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakichangia Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, walionyesha mshikamano mkubwa  kwa kushikilia shilingi kupinga bajeti hiyo kutengewa fungu dogo la fedha.

Bila kujadli itikadi zao vya vyama, Wabunge waishikama kwa kuihoji serikali na kusababisha kila mara mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, kusimama na kutoa ufafanuzi huku wakiwasihi wabunge hao kuachia msimamo wao.

Wabunge hao katika hoja yao wanapinga bajeti hiyo kupunguzwa kwa zaidi ya shlingi bilioni 100, ikizingatiwa kuwa maisha ya Watanzania yanategemea huduma bora ya afya.

Wanasema sekta ya afya ni muhimu kwa maisha ya watanzania hivyo, kuruhusu bajeti hiyo kupita ikiwa na mapungufu ni kuwahujumu ambapo mara nyingi wamekuwa wakiitwa kama ”muhuri” wa serikali.

Katika michango yao Wabunge walilalamika serikali kushindwa kulipa madeni ya ndani na nje kwa wakati na kutoa mfano wa deni  inalodaiwa na Bohari ya Dawa (MSD) la Sh. Bilioni 41.

Wabunge walilalamika hospitali nyingi nchini kukosa dawa, watumishi  kukosa mishahara kwa wakati, na vipimo muhimu kama X-ray kukosekana katika hospitali nyingi kutokana na wizara hiyo kutotengewa fedha za kutosha.

Akiwasilisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Dk. Seif Seleman Rashid Bunge kuidhinisha jumla ya Sh. 622,952,923,000.00. Kati ya fedha hizo, Sh. 317,223,431,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 305,729,492,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, inasema  haikuridhika na mtiririko wa fedha za bajeti ya wizara hiyo kwa kuwa hadi kufikia kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha ya bajeti hiyo zilikuwa hazijapokelewa na Wizara.

Mjumbe wa Kamati hiyo, Gregory Teu, wakati akisoma taarifa ya Kamati hiyo, analiambia Bunge kuwa takribani asilimia 53.84 ya bajeti hiyo zilikuwa hazijapokelewa na Wizara.

Wabunge walionyesha mshikamano wao wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti ya wizara hiyo baada ya Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Cecilia Paresso, kutishia kuondoa shilingi katika mshahara wa waziri, kama serikali isingetoa maelezo ya kuridhisha ya kupunguza bajeti ya wizara hiyo kutoka zaidi ya Sh. Bilioni 700 za bajeti ya mwaka jana hadi zaidiya Sh. Bilioni 600 zilizotengwa mwaka huu wa fedha.

“Mheshimiwa mwenyekiti natoa shilingi, na hoja yangu naomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono, tunatochotaka kujua ni uhalisia kwanini bunge lilipitisha shilingi bilioni 753 halafu serikali inatoa shilingi bilioni 357, je Watanzania watapate huduma ya afya,” anahoji.

Anasema Watanzania watakuwa wanamatumaini gani ya kupata afya wakati fedha zinazotengwa hazifiki wizarani.

Hoja hiyo ya Mbunge Paresso iliungwa mkono na wabunge wengi  ambapo tofauti na bajeti zingine, walikuwa na mshikamano kwa kushikilia shilingi bila kujali aliyeweka msimamo huo alikuwa ni wa kutoka chama gani.

Akiunga mkono  msimamo huo, Maria Hewa (Viti Maalum, CCM),  anasema wizara hiyo imefikia hatua hata ya kuacha mambo mengine muhimu, wazazi wanakufa kila siku na kuhoji  serikali ina vipaumbele vipi kama inaiacha wizara ya afya na kusisitiza lazima fedha itafutwe.

“Wabunge tuwe pamoja bila kujadili itikadi zetu, naomba mahala popote penye fedha, zitafutwe zipelekwe wizara ya afya, akina mama wanakufa,” anasema.

Pauline Gekul (Viti Maalu, Chadema),  anasema kupunguza  Sh. bilioni 100 kutasababisha majanga makubwa kwa wizara ambapo anasema janga la kwanza ni deni la MSD, vifaa tiba ,  na vituo muhimu vya kulelea wazee na watoto yatima kukosa fedha.

Kwa upande wake, Ester Matiku (Viti Maalum, Chadema), anasema kama serikali inajua kuwa haina fedha kwa nini inaweka kwenye vitabu, kwa kuwa mwaka jana ilitenga bilioni 753 na hadi Juni mwaka jana ilitoa bilioni 300 tu.

Anasema serikali ilitia saini Azimio la Abuja ambalo ndilo lengo la serikali katika kuboresha sekta ya afya, lakini mpaka sasa akina mama wajawazito wanakufa wakati kuna wanafanyakazi hewa wanalipwa karibu shilingi trilioni 1.2.

Aidha, anasema kama fedha hizo zingesimamiwa vizuri, zingepelekwa kwenye afya na kuweza kuepuka matatizo yanayoikabili wizara hiyo hivi sasa. Anapendekeza misamaha ya kodi ipunguzwe ili kuinusuru sekta ya afya.

Masoud  Abdalah Salum (Mtambile, CUF), anasema serikali siyo makini kwa kuwa Azimio la Abuja ilikubali yenyewe na inashangaza leo kwenda kinyume na azimio hilo.

Mary Mwanjelwa (Viti Malaamu, CCM), anasema sekta ya afya ni muhimu na Wabunge hawawezi kuwa na sauti ya kuongea kama hawatakuwa na afya bora.

Anasema kama Wabunge watapitisha bajeti ya wizara hiyo watakuwa hawaitendei haki wenyewe wala wananchi wanaowawakilisha.

“Sisi wanawake wote humu ndani naomba tuungane, sisi ndio wenye  uchungu wa kuzaa watoto, kila leo wanawake wanakufa na watoto, bajeti ya wizara ya afya iongezwe.”

Akiungana na Wabunge wenzeke, Zainab Zullu (Viti Maalum, CCM) , anasema wanawake hawapoo tayari kuona wenzao wanakufa kwa uzazi wakati Rais alishatoa tamko kuwa hataki kuona akina mama wanakufa kwa uzazi.

“Naiheshimu sana serikali yangu lakini katika hili naiomba iongeze pesa, hasa katika kuzuia vifo vya mama na watoto.”

Margareth Sitta (Viti Maalum,CCM) akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, naye anashikilia shilingi kwa kuitaka serikali iongeze pesa katika wizara hiyo muhimu.

Anasema hawawezi kuvumilia wakiona akina mama wakiendelea kupoteza maisha, hospitali zikosa dawa, wauguzi wakikosekana kwenye vituo vya afya, huku wizara hiyo ikikosa fedha kwa ajli ya kupata mahitaji muhimu kwa watanzania.

Hata hivyo, nguvu ya wabunge ilishindwa na serikali haikuongeza fedha hizo huku ikiahidi kwamba itakaa na kamati ya bajeti kuangalia namna ya kuziba mapungufu hayo.
 
CHANZO: NIPASHE

Related Posts