WANAFUNZI VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTUMIA BAISKELI

                                           Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
                                  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa
WANAFUNZI wa vyuo vikuu nchini wameshauriwa kutumia usafiri wa baiskeli kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani kwani kuendesha baiskeli si ushamba kama wengi wanavyodhani.

Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha Dodoma.
Alikuwa akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Stashahada Maalumu ya Sayansi, Hisabati na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Kauli hiyo ya Waziri ilikuja baada ya risala ya wanafunzi hao iliyosomwa na Charles Twinya kuomba kupatiwa usafiri kutokana na kutembea umbali mrefu kwenda madarasani na maabara hali inayopelekea kuchelewa vipindi, kuchoka hadi wengine kulala darasani. Alisema wamekuwa wakitembea kilomita mbili kutoka bwenini hata kufika madarasani.
Alisema wasaidiwe kupatiwa usafiri kama wanachuo wa Shahada huwa wakipanda magari.

Akijibu hoja hiyo, Waziri Kawambwa alisema umbali huo ni wa kawaida kwa wanafunzi hasa wanaosoma vyuo vikuu kwani pia ni sehemu ya mazoezi. Alisema kwenye nchi za Ulaya wanafunzi wamekuwa wakifika shuleni kwa kutumia baiskeli.