Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita huku akibubujikwa na machozi , mama huyo wa mtoto mmoja alisema anateseka kwa miaka miwili sasa na amehangaika katika hospitali nyingi kwa msaada wa watu bila mafanikio, hatimaye wamekata tamaa.
Akisimulia huku akitokwa machozi Aisha alidai: “Nimepooza kuanzia kiunoni hadi miguuni, mbaya zaidi miguu yangu kuna wakati inaniuma, inakuwa kama inapasuka hali ambayo imesababisha nishindwe kukaa achilia mbali kusimama.
“Nilikuwa na mume ambaye alikuwa akinipenda sana nami kumpenda na tukafanikiwa kumpata mtoto mmoja huyu (akamshika) Afsa, baada ya miezi kadhaa ya kuumwa, mume wangu akaingia mitini na kutuacha tukitaabika kwa njaa na ugonjwa.
“Baada ya mume kunikimbia mimi na mtoto wangu mwenye miaka minne tunasaidiwa na majirani na ….” Hakumaliza alichotaka kusema akawa anatokwa machozi huku akilia kwa kwikwi.Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasilina na mama huyo kwa namba 0654 565423 au 0755 45 87 93.