KIPIGO KINAWEZA KUMNYOOSHA MWENZI WAKO?

Mwaka mpya huoo umeshaanza kuyoyoma! Vipi hali yako msomaji wangu wa uwanja wetu huu mzuri! Nakukaribisha kwa moyo mkunjufu tujadili mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.

Suala la wanandoa au wapenzi kupigana siyo geni, huenda hata wewe unafanya au unafanyiwa, au pengine hata usiku wa jana umeshuhudia jirani, ndugu au rafiki yako akimpiga au kupigwa na ampendaye.

Vipigo kwa watu wawili wa jinsia tofauti wanaoishi pamoja kwenye uhusiano wa kimapenzi, iwe ni kwenye ndoa, uchumba au mapenzi yasiyo rasmi, vimekuwa ni fasheni na kwa hapa nyumbani, wanawake wanaonekana kunyanyasika zaidi kutoka kwa wenzi wao ingawa pia ipo idadi ndogo ya wanaume wanaopigwa na wake zao.
Nataka tujadiliane, kuna ulazima wowote wa kunyanyua mkono wako na kumpiga mwenzi wako kwa sababu amefanya kosa hili au lile? Ni sawa kumpiga mwenzi wako hadi kumjeruhi vibaya au pengine hadi akapoteza fahamu? Kuna faida yoyote ya kufanya hivyo?
NI MUHIMU KUJIFUNZA
Mwanaume unapofikia hatua ya kukomaa kimwili na kiakili, unahitaji mwenza wa kuishi naye na kujenga familia. Huhitaji bondia mwenzako wa kurushiana naye masumbwi wala huhitaji gunia la mazoezi la kujifunzia kupiga kila unapojisikia bali mke mwema (wife material).
Unahitaji mke ambaye atakulea wewe na watoto mtakaojaliwa kuwapata, nawe utamtunza na kumtimizia mahitaji yake yote muhimu. Tafsiri ya ndoa, ni pale wawili mnapoamua kuwaacha wazazi wenu na kuungana kujenga familia moja, mkiunganishwa kwa upendo wa dhati na amani.
Kwa hiyo tunachojifunza hapa ni kwamba mwanaume unapoamua kuoa, siyo kwamba unatafuta mtu wa kumtumikisha na kumpeleka vile unavyotaka wewe, eti kwa sababu tu yupo chini yako na wewe ndiye uliyelipa mahari au kugharamia sherehe za ndoa yenu.
Anapoamua kuwaacha wazazi wake na kila kitu alichokizoea na kuja kwako, anakuwa na mategemeo makubwa kwamba atakuwa kwenye mikono salama, utampenda na kumtunza kama mboni ya jicho lako lakini mbona mkishaingia kwenye ndoa, mkishazaa na kuzoeana unaanza kumgeuza kuwa ngoma au gunia la mazoezi?
Nazungumza na wewe mwanaume mwenye tabia ya kumtwanga mwenzi wako bila huruma. Wakati unamchukua kwa wazazi wake uliahidi kuwa utakuwa unambonda kila siku akikukosea?
Yawezekana kila siku ulikuwa unakosea kwa kumbonda mwenzi wako, pengine ulikuwa umejisahau au hujui madhara yake, naomba mada hii iwe taa nyekundu kwenye kichwa chako. Wanaume waliostaarabika, wanaojua mapenzi, kujali na kutunza, hawaendekezi vitendo vya ukatili kwa wenzi wao.
Achana na baadhi ya mila za makabila fulani ambazo eti kama mke hapigwi, tafsiri yake ni kwamba hapendwi. Sitaki kuzungumzia huko kwa sababu naheshimu mila na desturi za kila mmoja.
WANAWAKE WANAJITAKIA KUPIGWA?
Ipo imani katika jamii kwamba mara nyingi wanawake ndiyo huwa wanajitakia wenyewe kupigwa kutokana na jinsi wanavyoishi na waume au wenzi wao. Kwamba yapo matendo yanayofanywa na wanawake ambayo hata ukiwa na roho ya upole kiasi gani, lazima ipo siku hasira zitavuka mipaka na kujikuta ukimshushia kipigo kikali.
Sitaki kuunga mkono moja kwa moja imani hii ingawa naamini pia siyo kila mwanaume anapenda kumpiga mwenzi wake, pengine kama baadhi wanavyosema, kuna wanawake wanakuwa wanajitakia wenyewe kupigwa, iwe ni kwa kujua au kwa kutokujua.
Mimi si mjuzi wa kila kitu ila naamini tukijadiliana na wewe msomaji wangu, tutafikia hitimisho zuri kabisa. Je, kwa mtazamo wako unaona ni sahihi kumpiga mwenzi wako? Je, unajisikiaje unapopigwa hadi kuumizwa na mwanaume unayempenda? Kuna athari au faida gani za kupigana?
Kuwa huru kuchangia mawazo yako kupitia kwa namba za hapo juu na wiki ijayo, tutaendelea na mada yetu.