DUDE "2014 NI MWAKA WA MAJANGA KWANGU"

TUKIWA tunaelekea ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa ni mwaka wa majanga kwake hivyo anamuomba Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake.

Akipiga stori na paparas wetu, Dude alisema ndani ya mwaka huu hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya yale aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo linamuumiza kwani alitegemea kufanya mambo mengi lakini hakufanikisha.

“Nilitegemea kufunga ndoa lakini imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.