Mwanaume mmoja anayesemekana ni mfanyabiashara ambaye pia anatajwa kugombea udiwani wa kata moja iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, aliyetajwa kwa jina moja la mzee Beno amenaswa akiwa chumba cha gesti na mwanafunzi wa chuo kimoja kilichopo Kibamba jijini Dar.
Tukio hilo la aina yake lilijiri Oktoba 20, mwaka huu ndani ya gesti moja iliyopo Kimara-Suka jijini Dar es Salaam ambako mama mzazi wa wa binti huyo ndiye aliyemnasa mheshimiwa mtarajiwa huyo na binti yake.
Awali, mama huyo alisema alianza kuwa na wasiwasi na mwenendo wa binti yake huyo kutokana na kuanza kale katabia ka’ kuchelewa mara kwa mara kurudi nyumbani akitoka chuoni, akajiongeza!
Kwa mujibu wa mzazi huyo aliyeonekana kufura kupita tafsiri ya neno lenyewe, alianza kibarua cha ushushushu kama si upelelezi wa kumfuatilia binti yake ambapo siku moja aliifanyia udukuzi simu yake na kukuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenye simu hiyo ukimtaka afike kwenye gesti hiyo.
Ikadaiwa kuwa, mbali na SMS hizo, mama huyo aliwahi kumsikia binti yake akiwa hewani na ‘mheshimiwa’ huyo jambo lililozidisha hasira zake kama mama akiamini kuna mwanaume anamharibu binti yake aliye na malengo naye mazuri siku za usoni.
Ndipo mama huyo akamuweka kikao kifupi binti yake na kumtaka aseme ukweli kuhusu mtu aliyemuita gesti Kimara-Suka.
———–
Mazungumzo yao:Binti: “Mtu gani mama?”Mama: “We’ usinitanie, nimekuta meseji kwenye simu yako, kuna mwanaume umemsevu kwa jina la Sweet, amekuita gesti, ni nani?”Binti: “Aaah! Ni mzee mmoja hivi.”Mama: “Anaitwa nani?”

Binti: “Anaitwa mzee Beno.”
Mama: “Ni mpenzi wako?”
Binti: (moyoni) “mama bwana, sasa si umeona nimemsevu Sweet anaweza kuwa mjomba ‘angu kweli? (kwa sauti) “ndiyo mama lakini sijawahi kufanya naye chochote hata siku moja.”
Mama: “Apia.”
Binti: “Hakyamungu vile.”
———————————-
Ikadaiwa kuwa baada ya hapo, binti akatakiwa kumjibu mzee huyo kwamba anakwenda wakutane huko gesti ili wamalizane kwani ‘amemmisi’ sana siku hiyo, mzee akashindwa kujiongeza.
Binti akiwa na mzazi wake na skwadi nyingine walianza safari ya kwenda Kimara –Suka kwenye gesti hiyo ambapo walikaa baa ya jirani, binti akaenda ndani ambako mzee huyo alishafika zamani na kumsubiri.

Baada ya muda, binti alituma meseji kwa mama yake akisema mambo tayari, wapo ‘weupe pee’ (hawana nguo). Ndipo mama huyo akachukua timu yake na kuvamia gesti hiyo kwa ajili ya kulianzisha.
Huku akiwa amekaa kwa tafakuri ya kina baada ya kufumaniwa, mzee Beno alisema ameumbuka na kuitaka familia ya mwanafunzi huyo kumalizana kifamilia nje ya gesti hiyo.