Ndege za kijeshi kutoka Marekani zimetekeleza mashambulizi tisa ya angani dhidi ya wanamgambo wa Islamic State kazkazini mwa Iraq ili kuvisaidia vikosi vya Iraq kuliteka bwawa moja muhimu karibu na mji wa Mosul.
Bwawa hilo ndio kubwa nchini humo na lilitekwa na islamic state mapema mwezi huu.
Makamanda wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi hayo yalioanza ijumaa usiku yaliharibu zaidi ya magari 14 ya kivita yanayomilikiwa na Islamic State.
Duru mjini Mosul zimearifu kuwa takriban wapiganaji kumi na moja wanadaiwa kuuawa katika shambulizi hilo.
Jenerali mmoja wa vikosi vya Kikurdi kazkazini mwa Iraq amesema kuwa vikosi hivyo vimeanzisha mashambulizi ya kuliteka bwawa hilo