Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu yaahidi Kulipa Fedha za Mafunzo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu

        HESLB

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), imesema mwishoni mwa wiki hii, itakuwa imelipa fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata fedha hizo kwa mwaka 2013/14.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/15.
Alisema bodi hiyo ilikwama kuwalipa baadhi ya wanafunzi walioanza mafunzo kwa vitendo Julai mwaka huu kutokana na uhaba wa fedha.
 
Aliongeza kuwa, hadi sasa vyuo vitano ndivyo ambavyo wanafunzi wake hawajapatiwa fedha hizo, lakini hadi mwishoni mwa wiki hii, fedha hizo zitakuwa zimeingizwa kwenye akaunti zao.
 
Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Tumaini Makumira Arusha (TUMA), Chuo cha Mtakatifu Stefano Moshi (SMMUCO), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mtakatifu Agustine Mwanza na Chuo cha Theophil Kisanji (TEKU), ambapo jumla yao wapo wanafunzi 9,946.
 
Katika hatua nyingine, Mwaisobwa alisema hadi wanafunga maombi ya mikopo Julai 31 mwaka huu, wamepokea maombi ya mikopo 58,037 kati ya hiyo, wavulana 37,689 na wanawake 19,592,” alisema.
 
Alisema baada ya kufungwa rasmi mchakato wa kupokea maombi hayo, hatua inayoendelea ni uhakiki wa taarifa za waombaji na kupitia nyaraka mbalimbali ambazo zimeambatanishwa na waombaji.
 
“Mchakato wa kuchambua maombi yao, utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) ili kujiunga na vyuo mbalimbali yatakapowasilishwa kwenye bodi ya mikopo,” alisema Mwaisobwa.
 
Aliongeza kuwa, udahili wa wanafunzi unaofanywa na TCU kwa mfumo wa pamoja, unajulikana kama(CAS) ambao hutumiwa na vyuo vyote vya Elimu ya Juu na ambao hawako kwenye mfumo ili kutunza majina ya wanafunzi waliodahiliwa waweze kuthibitishwa kabla ya kupatiwa mikopo.
 
Agosti 15 mwaka huu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar es Salaam, liliweka ulinzi mkali katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo hususan kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ili kudhibiti maandamano ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu waliotaka kuandamana kwenda ofisini kwa Waziri Mkuu ili wapate majibu ya fedha hizo.
 
Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (TAHLISO), ilitangaza maandamano hayo ya amani ili kuishinikiza Serikali itoe majibu au kuwapatia fedha wanafunzi ili wakamilishe muhula wa masomo kwa mafunzo ya vitendo.