Stars yabomoka kiungo, Nooij apasua kichwa

                      kocha Mholanzi, Mart Nooij
Wakati safu ya kiungo ya timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), ikiwa imezidi kudhoofika kufuatia kuumia kwa Jonas Mkude na Himid Mao, huku Frank Domayo akiwa anauguza jeraha za upasuaji wa paja, kocha Mholanzi, Mart Nooij, ameonyesha wazi hofu yake dhidi ya wapinzani wao Msumbiji katika kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika.

Nooij amesema anawafahamu vyema Msumbiji na hawezi kuahidi chochote kuhusu matokeo katika mechi yao hiyo ya raundi ya pili ya mtoano itakayofanyika Julai 20 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Daktari wa StarsBilly Haonga, alisema bado haijajulikana kama Mao na Mkude wataweza kuivaa Msumbiji.

Haonga ambaye ni daktari bingwa wa mifupa, alisema hatma ya nyota hao wawili itajulikana baada ya majibu ya vipimo kutoka. Daktari huyo alisema kuwa yeye ndiye aliyeokoa maisha ya soka ya Domayo baada ya kumbaini ana jeraha katika msuli na kushauri afanyiwe upasuaji mapema na hatimaye atarejea uwanjani salama.

Hata hivyo, Nooij alisema jana kuwa kikosi hicho kimefanya maandalizi mazuri nchini Botswana na leo kinaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Tukuyu mkoani Mbeya kuendelea na kambi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo.

Nooij alisema kuwa anawajua vizuri wapinzani wake Msumbiji na anaamini Stars itautumia vyema uwanja wa nyumbani na kuwataka mashabiki wasiwe na hofu.

"Nawajua (Msumbiji), na wao wananijua, ule uwanja unaingiza mashabiki 60,000 lakini natarajia Julai 20 mashabiki wawe 70,000 kushuhudia mchezo huo muhimu," alisema.

Kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen, alikataa kuahidi lolote kuelekea katika mchezo huo na ule wa marudiano utakaofanyika baada ya wiki mbili.

Aliongeza kwamba kikosi hiko kitakuwa kinafanya mashambulizi ya kushtukiza na kutowapa wapinzani wao nafasi ya kujipanga ili kuwazuia wachezaji wake watakapokuwa wanatengeneza nafasi za kufunga.

Nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro' alisema kuwa kikosi chao kimejipanga kusaka ushindi katika mechi hiyo ya kwanza ili kujiweka kwenye mazingira ya kusonga mbele.

Cannavaro alisema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu, wachezaji watahakikisha wanacheza kwa bidii ili kuwafunga Msumbiji na kuwashangaza wale ambao hawaiamini timu hiyo.

Alieleza kuwa licha ya kupoteza mechi mbili za kirafiki na kushinda moja huko Botswana, timu hiyo imejifunza mambo mengi na itapunguza makosa katika mechi hiyo ya mashindano.

Stars inakutana na Msumbiji baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2, ikipata ushindi wa bao 1-0 nyumbani na sare ya 2-2 mjini Harare.

Mshindi kati ya Stars na Msumbiji atatinga Kundi C la kuwania kwenda kwenye fainali za Afrika 2015 nchini Morocco lenye timu za Zambia, Cerpe Verde na Niger. Timu mbili kutoka kila kundi zitaenda kwenye fainali hizo pamoja na timu moja ya tatu iliyofanya vizuri zaidi zitakazoungana na wenyeji Morocco katika fainali hizo.

Wakati huo huo, Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa tayari shirikisho hilo limeshaandika barua ya kuwaita wachezaji watatu wa kimataifa ambao Nooij amewaita kuivaa Msumbiji.

Wambura aliwataja nyota hao kuwa ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, wote wanacheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mwinyi Kazimoto aliyeko Qatar.

KIINGILIO BUKU 7
TFF ilisema jana kuwa kiingilio cha chini katika mechi ya kwanza kati ya timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayofanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa ni Sh.7,000.

Wambura alisema kuwa kiingilio cha juu kwa viti maalum itakuwa ni Sh.100,000, na kwa mashirika yatakayohitaji tiketi za wafanyakazi wake watalipia Sh.50,000 kwenye eneo hilo.

Wambura alisema kuwa tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa mapema kwa njia ya Maxi Malipo na anawashauri mashabiki wa soka nchini kununua mapema tiketi hizo ili kuepuka usumbufu.