Polisi wawapiga risasi wacheza vigodoro

Polisi jijini Dar es Salaam wanadaiwa kuwapiga risasi wanawake wawili ambao walikuwa ni miongoni wa wacheza ngoma maarufu kwa jina la 'kigodoro'.

Tukio hilo limetokea juzi jioni maneo ya Mwanyamala jijini Dar es Salaam na wanawake ambao wamejeruhiwa ni Zawaiya Hamisi na Gile Roy wote wakazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Wakati Zawaiya akijeruhiwa kwenye makalio na kiunoni, Gile ameripotiwa kujeruhiwa juu yapaja.Akizungumza nyumbani kwake Mwananyamala mmoja wa majeruhi hao Zawaiya amesema kuwa alipigwa risasi akiwa amekaa pembeni akiangalia askari polisi walipokuwa wakitumia nguvu kuwakamata wapiga ngoma na matarumbeta.

"Mimi ni mmoja wa wacheza ngoma, na ilikuwa ni harusi ya shoga yangu kwa hiyo ilinihusu, lakini tulipofika sehemu tulivamiwa na kundi la askari polisi waliokuwa wamechanganyika na polisi jamii na kuanza kutuhoji ni kwa nini tunacheza vigodoro wakati vimepigwa marufuku," alisema majeruhi huyo.

Alisema waliwajibu askari hao kuwa wanavyojua ni kwamba ngoma ya vigodoro imekatazwa usiku na si mchana kweupe kama muda ule waliokamatwa.
"Ilikuwa ni saa tisa hivi kuelekea saa kumi, jamani muda huo kweli ni mbaya na kibali tunacho, tukaona kama ni uonevu na kuna watu walioingilia kati kututetea, baadhi yao walikamatwa," alisema.

Alisema kuwa awali alitaka kukimbia, lakini alihakikishiwa usalama na askari mmoja, akasimama kando, lakini baadaye alijikuta akipigwa risasi na askari wengine ambao walikuwa wanatumia nguvu kutaka kuwakamata wapiga ngoma na matarumbeta.

"Nilihisi kama ganzi hivi, nikaanguka chini, sikujua nini kimetokea, lakini baadaye nikaona damu zinanitoka ndiyo nikajua kuwa nimeumia," alisema Zawaiya.Alisema kuwa alisikia sauti za risasi sita zikipigwa kabla ya yeye kupigwa.

"Nilipelekwa kwenye hospitali ya Mwananyamala na kutibiwa pamoja na mwenzangu lakini hatukulazwa," alisema.Muuguzi wa hospitali hiyo alithibitisha kupokea majeruhi wa risasi kwenye hospitali hiyo.

"Hao kinadada waliletwa jana jioni na watu walijaa sana hapa, lakini kwa sasa hawapo," alisema muuguzi huyo.

Shuhuda wa tukio hilo Ahmed Mudhihiri alisema kuwa kilichotokea ni askari polisi kutumia nguvu kubwa kwa jambo dogo tu.

Mudhihiri ambaye pia ni Katibu Kata wa Chama Cha Wananchi (CUF) kata ya Kinondoni zilizopo Mwananyamala, alisema kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya ofisi zao wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha kata.

Alisema yeye ni mmoja wa watu waliotoka nje kwenda kuwatetea kinamama hao na kundi lao la ngoma waliokuwa wamezingirwa na askari, lakini kilichotokea ni kwamba askari walipiga risasi hovyo zilizowapata baadhi yao.

"Kuna wenzetu wawili walikamatwa," alisema Mudhihiri na kuongeza."Hata kama wamefanya makosa, lakini sidhani kama ilipaswa kutumia nguvu kubwa kiasi kile, ni uonevu mkubwa," alisema.

Baadhi ya askari wa kituo kidogo cha Polisi Mwinjuma, walithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wakasema waliokuwa kwenye operesheni hiyo ni askari wa kata.

Walisema kuwa kilichotokea ni kwamba askari hao walitaarifiwa kuwa kuna kinadada waliokuwa wakicheza ngoma ya kigodoro mchana kweupe kwa kuvua nguo mbele za watoto wakati serikali imeshapiga marufuku.

Askari hao ambao hawakutaja majina yao kwa sababu si wasemaji wa Jeshi la Polisi, walimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa, wenzao walipofika hapo na kuwazingira ili kuwaweka chini ya himaya na kuwapa somo, walikumbana na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya watu hasa vijana ambao walianza kuwarushia mawe na silaha nyingine za kienyeji.

"Askari hawakuwa na nia mbaya, walitaka kuwaambia wasicheze utupu kwa sababu kulikuwa na watoto pale na ni kinyume cha sheria hasa ikizingatia bado mchana, lakini wakaanza kupigwa mawe, ilibidi wapige risasi kadhaa juu ili kuwatawanya kwa sababu hali ilishakua mbaya," alisema mmoja wa maafande hao.

Wakasema kuwa wanawake hao walijeruhiwa kwa bahati mbaya na wala si dhamira ya polisi, ila ni kwa sababu watu walikuwa wengi, hivyo zilipoanguka chini ziliwapata baadhi.

"Ndugu yangu, kama askari wangepiga kwa nia ya kumdhuru mtu kwa sehemu ambazo wamejeruhiwa sidhani kama wangekua hai," alisema mmoja wa maafande.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.
CHANZO: NIPASHE