Nyasi za viwanja mbalimbali kuanza kuwaka moto Septemba 20, Ligi Kuu Bara

Shirikisho la Soka nchini (TFF), limetangaza rasmi msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaanza Septemba 20 badala ya Agosti 24, mwaka huu kama ilivyotangazwa awali.

Taarifa iliyotolewa na TFF jana jioni baada ya tetesi za ligi hiyo kusogezwa mbele kuvuja, ilieleza shirikisho limelazimika kuisogeza ligi hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kupisha michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Hata hivyo, mashindano ya Kombe la Kagame ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanza Agosti 9--23,  jijini Kigali, Rwanda, nayo yanafanyika nje ya kalenda yake ya kila mwaka.

Mashindano ya Kombe la Kagame yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), hufanyika kila mwaka kati ya Mei na Juni lakini mwaka huu yalisogezwa mbele hadi Agosti ili kupisha fainali za Kombe la Dunia, sababu nyingine ikiwa ni kukosekana kwa wadhamini.

Yanga ndiyo wawakilishi wa Tanzania Bara katika mashindano hayo ya Cecafa, ambayo mwaka jana ilishindwa kwenda Sudan kutetea ubingwa wake ilioutwaa 2012 baada ya kuzuiwa na serikali kutokana na hali ya amani ya nchini humo kutokuwa shwari.

 "Ligi imesogezwa mbele hadi Septemba 20 kwa sababu mbalimbali ikiwamo kupisha mashindano ya Kombe la Kagame," ilisema kwa kifupi taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura jana jioni.

Alizitaja timu 14 zinazotarajiwa kushiriki ligi hiyo kuwa ni pamoja na bingwa mtetezi Azam, CoastalUnion, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.

Ligi hiyo ndiyo inayotoa wawakilishi wa Bara katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho na Kombe la Kagame.