Mabinti Watanzania wanavyotumikishwa madanguroni China

Taarifa zinazomuhusu binti wa Kitanzania Munira Mathias (siyo jina lake halisi) ambaye alipelekwa China kwa ahadi ya kupewa kazi hotelini, lakini alipofika hadithi iligeuka na alianza kutumikishwa katika biashara ya ukahaba.
Munira baada ya kuamrishwa na ‘bosi’ wake kufanya kazi hiyo, alielekezwa na wenzake kwenda eneo la soko liitwalo Chambu Chambu ambako wanawake Watanzania wanafahamika kuwa maarufu kwa biashara ya ukahaba.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 23 anasema usiku wa kwanza alipokwenda sokoni Chambu Chambu, wenzake walimkimbia, hivyo alichanganyikiwa na kuanza kuwapigia simu wenyeji wake kwani hakujua la kufanya.
“Nilimpigia simu Jacky na yeye alinijibu, ‘acha ujinga, tafuta hela uniletee mimi.” Anasema katika mazingira hayo alianza kulia na wakati akilia, alikutana na mwanaume wa Kinigeria, ambaye alimhoji maswali kadhaa.
Mnigeria yule alisema anaifahamu hoteli anayoishi Munira, lakini alimtaka wazungumze kwanza biashara kisha ampeleke na Munira alikubali.
“Nilizungumza naye biashara na tukakubaliana twende kwenye hoteli niliyofikia, baada ya kufanya mapenzi akanilipa  Dola 100, baadaye nilidakwa na mwenyeji wangu akinitaka nimpe fedha zote nilizopata,” anasema.
Alipomkabidhi fedha hizo, aliamrishwa kurudi tena sokoni kutafuta kiasi kingine cha fedha hadi atimize dola 200. Wakati huo bado ulikuwa ni mchana.
“Baada ya kumalizana na Mnigeria yule, nilienda kulala, lakini sikulala sana kabla mwenyeji wangu hajaniamsha na kuniambia lazima nitimize Dola 100 iliyobaki, hivyo nikanyanyuka na kwenda tena sokoni,” anasema.
Munira akawa hali wala halali vizuri akifanya kazi ya kujiuza mwili wake, kazi ambayo hata kiasi kidogo alichopata alitakiwa kugawana na mwenyeji wake kwa kumpatia Dola 200 kwa siku.
“Nilikuwa nachoka, hasa kwa kudaiwa, wakati mwingine nikiwa kwenye siku zangu najiuliza nitafanyaje ili nipate fedha za kulipa deni? Niliondoka hapa nikiwa na afya, lakini nilipofika huko baada ya muda mfupi niliisha, yaani niliisha,” anasema.
Ukatili wa aina yake
Anasimulia kwamba, siku moja  saa 10.00 usiku akiwa klabu,  alijisikia vibaya akatoka nje, akiwa huko alikutana na mwanamume ambaye walikubaliana wakastarehe kwa ujira fulani. 