Mzozo umeibuka kwenye Bunge la Indiabaada ya kuwepo Ripoti kuwa baadhi ya Wabunge wa dini ya Hindu walijaribu kumshurutisha mtu mmoja aliyekuwa kwenye mfungo wa Ramadhan kula chakula.
Wabunge hao kutoka mrengo wa kulia wa Chama cha Shiv Sena wameripotiwa kuwa walikuwa na hasira kwa kuwa hawakupatiwa chakula walichokichagua katika mgahawa wa Serikali.
Waislamu duniani kote wanafunga kula na kunywa kabla yajua kuzama katika kipindi cha mfungo.
Vyama vya upinzani vikiongozwa na chama cha Congresswamekemea kitendo hicho wakisema ni ukiukwaji wa imani ya dini,na kutaka chama cha Shiv Sena kuomba radhi
Kwa mujibu wa Ripoti, tukio hilo lilitokea jumanne mjini Delhi baada ya wabunge kadhaa kutoka chama cha Shiv Sena cha jimbo la Maharashtrakuchukizwa na hali ya kutokuwepo kwa chakula walichokitaka na kutumia nguvu kusokomeza kipande cha mkate mdomoni mwa mfanyakazi wa mgahawa aliyekuwa katika mfungo.