Dk Slaa: Sitosahau siku nilipopigwa mabomu na Polisi

Kushushwa juu ya  fuso na mabomu kwenye kebini umebaki peke yako watu wote wamekimbia. Ndiyo wamekimbia...nimebaki na mlinzi wangu tu pale juu ya gari. Polisi walipoona vile walinifuata na kunirushia mabomu ya machozi na kunifanya nishindwe kupumua kwa dakika tano mfululizo.”
Hii ni sehemu ya ushuhuda wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuhusu  misukosuko ya maisha yake kisiasa.
Ni sehemu ndogo iliyojaa taswira ya ukatili, lakini pia nguvu ya ushindi katika harakati za kawaida za kuleta mapinduzi.
Kwa wengi wanaomfahamu Dk Slaa na mambo ambayo hukumbana nayo huenda wasiupe uzito ushuhuda huo, lakini kwa kiongozi huyo machachari aliyegombea urais mwaka 2010 na kushindwa na Rais Jakaya Kikwete wa CCM, hilo ndiyo tukio ambalo anasema hatalisahau katika maisha yake yote kwa sasa.
 “Baadaye nikamwambia mlinzi wangu hebu tuteremke huku juu...na polisi walipoona vile wakatufuata tena na kuendelea kutumiminia risasi, nikaona watatuua.  Vijana wangu walipoona vile wakaniambia Dokta ruka!
”Sasa narukaje kutoka kwenye kebini hadi chini? hapa mimi nikawaeleza nitateremka vipi wakaniambia mzee serereka...bahati nzuri nikaserereka na ule mlango na nilipofika nusu wakaniambia ruka.
“Nilipofika katikati nikaruka, kumbe chini yagari kulikuwa na vijana wawili nao wamejificha pamoja na mlinzi wangu, tukawa wanne.”
Hii ni simulizi ya Dk Slaa wakati akijibu swali aliloulizwa katika mahojiano maalumu na gazeti hili wiki iliyopita kuhusu ni  jambo gani la kusikitisha ambalo hatolisahau kwa umri wake hasa tangu alipotoka  upande wa pili (upadri) kuingia katika siasa.
Anajibu kuwa ilikuwa ni mkutano uliofanyika Novemba 8 kuamkia Novemba 9 mwaka 2011 ambao ulifanyika Arusha wakati Mbunge wa Jimbo hilo, Godbless Lema alipovutana na polisi kuhusu kutoka kwake mahabusu na siku hiyo ilikuwa Lema aachiwe na wananchi walijitokeza kwa wingi mahakamanikusubiri kuachiwa kwake.
Baada ya kuona umati huo polisi wakapeleleza nani anaweza kuondoa umati huu, wakaambiana,  Dk Slaa au Mbowe (Freeman Mbowe- Mwenyekiti wa Chadema aliyekuwa Arusha), wakaona wanipigie simu na mimi nilikuwa chuo kimoja kilichoko Usa River Arusha natoa mada. Nikawaeleza siwezi kuja, wakaniuliza hadi saa ngapi nikawaeleza hadi saa tisa wakakubali wakaniambia tutakusubiri dokta.
Wananchi walikuwa wengi siku hiyo baada ya kusikia kwamba Lema ataachiwa. Nilipofika nilikuta umati mkubwa sana wa watu hadi nikaogopa kwa kuwa sikuwa hata na vipaza sauti, hivyo nikajiuliza nitawahutubiaje wananchi hawa na wanisikie?
Siku hiyo baada ya mvutano wa Lema na polisi hawakuwa wamemleta mahakamani na wananchi walijua yupo wamemfungia, jambo lililozua vurugu lakini nilipofika polisi wakanieleza tuwapeleke wapi wao wakasema tuwapeleke uwanjani.