Watu wenye silaha wamemuuwa kiongozi wa kiislam Mombasa akiwa ni kiongozi wanne wa kidini kuuwawa mjini humo katika miaka miwili iliyopita.
Polisi wanasema sheikh Mohamed Iddriss mwenyekiti wa baraza la Maiman na Wahubiri Kenya alipigwa risasi na kuuwawa nje ya msikiti jumanne asubuhi.
Viongozi watatu wa kiislam waliouwawa mapema katika mji huo walishutumiwa kwa kuwa na mahusiano na kundi la alshabab lenye mahusiano na alqaeda lililopo Somalia.
Vikosi vya kijeshi vya Kenya viko Somalia vikipambana na wanamgambo wa Somalia ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi Kenya hasa lililokuwa kubwa sana la maduka ya kifahari ya westgate huko Nairobi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 60 waliuwawa.